Chama hicho kimekishinda chama cha kitaifa cha Geert Wilders kilichokuwa dhidi ya wahamiaji na Uislam kwa kura nyingi kuliko ilivyotarajiwa.
Wakati zaidi ya nusu ya kura zikiwa tayari zimehisabiwa, Kituo cha Rutte cha mrengo wa kulia cha chama cha People’s Party for Freedom and Democracy kinatarajiwa kuchukua viti 32 kati ya 150, kitakacho kuwa kinaongoza kuliko chama chochote kingine.
Vyama vitatu vinatarajiwa kushinda viti 19 kila kimoja, kikiwemo chama cha Wilders’ anti-immigration Freedom Party, na chama cha Christian Democrats na Chama cha D66.
Muundo mpya wa Bunge utatangazwa pamoja na matokeo rasmi Machi 21.
Maafisa wanasema watu wengi walijitokeza kupiga kura zaidi kuliko wakati wowotekatika miongo mitatu iliopita, na kufikia asilimia 81.