Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 09:58

Ruto ataka ushirikiano zaidi Afrika Mashariki


william ruto

Naibu wa rais wa Kenya William Ruto amewataka viongozi katika Jumuiya ya afrika aashariki - walio serikalini na wa upinzani - kuangazia faida za soko la jumiya ya afrika mashariki, SADEC na COMESA na wala sio maslahi binafsi ya nchi zao kiuchumi.

Ziara ya William Ruto Uganda
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:56 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Akizungumza katika hafla ya maombi ya taifa nchini Uganda Alhamisi, Ruto amesema kwamba kizingiti kikubwa cha maendeleo katika jumuiya ya Afrika Mashariki ni ubinafsi. Serikali ya Uganda nayo imeitaka Kenya kutilia maanani kiwango cha bidhaa zake zinazoingia nchini humo kabla ya kuzuia bidhaa zake hasa sukari, kuingia soko la Kenya.

Ruto alisema Jumuiya Afrika mashariki ina kila aina ya rasilimali zinazoweza kuinua uchumi wa nchi hizo katika kiwango ambacho kitagusa mapato ya watu binafsi katika eneo hilo.

Naibu rais huyo wa Kenya ametaka viongozi wa nchi hizo kuwacha mivutano ya kibinafsi na kuangalia zaidi jinsi wananchi katika eneo zima wanavyoweza kufaidika na ushirikiano wa serikali zao.

XS
SM
MD
LG