Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 06:46

Ruto akosoa jamii ya kimataifa kuhusu Daadab


Naibu wa Rais wa Kenya william Ruto (kulia) anasalimiana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, katika makao makuu ya Umoja huo mjini New York tarehe 19 Septemba, 2016.
Naibu wa Rais wa Kenya william Ruto (kulia) anasalimiana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, katika makao makuu ya Umoja huo mjini New York tarehe 19 Septemba, 2016.

Na BMJ Muriithi

Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto, siku ya Jumatatu aliikosoa jamii ya kimataifa kwa kile alichokiita ukosefu wa uwajibikaji kuhusiana na mzozo wa wakimbizi barani Afrika.

Akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi na serikali uliofanyika katika ukumbi wa umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Ruto alisema kuwa Kenya imeonyesha ukarimu mwingi kwa wakimbizi walio kwenye kambi ya Daadab, na kwamba sasa ni wakati mwafaka kwao kurejea makwao.

Ruto alikuwa mmoja wa waliozungumza katika kikao kilichoitishwa kwa minajiri ya kutafuta suluhisho la kudumu kwa mzozo wa uhamaji wa halaiki ya wakimbizi kutoka maeneo yaliyokumbwa na vita na migogoro ya kisiasa, zikiweno nchi za Syria na Somalia.

Alisema msimamo wa kenya wa kuwahamisha wakimbizi hao hautabadilika na kuhoji ni kwa nini mikutano ya viwango vya juu kuhusu swala la wakimbizi hufanyika na ili hali mengi ya mataifa ya yanayoahidi kutoa misaada hayatimizi ahadi hizo.

Alitaja changamoto zinalzoletwa nauhifadhi wa wakimbizi kama vile ukosefu wa usalama na kusema kuwa shambulizi la kigaidi la miaka mitatu iliyopita - Westgate - lilipangwa katika kambi ya Daadab.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon, alizitaka serikali za nchi wanachama ywa umoja huo, kuonyesha nia ya dhati ya kukabiliana na mzozo wa wakimbizi ambao, alisema, umefika viwango vibaya zaidi tangu vita vya pili vya dunia.
kikao cha 71 cha Umoja wa mataifa kilianza Jumatatu na kilitarajiwa kufunguliwa rasmi siku ya Jumanne.

Kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu, marais wa Kenya, Tanzania na Uganda hawakuhudhuria kongamano la mwaka huu na badala yake kuwatuma wawakilishi. Rais wa Uganda Yoweri Museveni yuko ziarani Ufaransa huku mabwana Magufuli na Kenyatta wakisalia nchini mwao mtawalia.

XS
SM
MD
LG