Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 11:34

Ruto apinga pendekezo la kuondoa mihula 2 ya rais katika katiba


Rais wa Kenya Dkt. William Ruto akiwapungia mkono watu waliojitokeza wakati wa kuapishwa kwake katika uwanja wa michezo wa Kasarani, Nairobi Sept 13, 2022
Rais wa Kenya Dkt. William Ruto akiwapungia mkono watu waliojitokeza wakati wa kuapishwa kwake katika uwanja wa michezo wa Kasarani, Nairobi Sept 13, 2022

Raisi wa Kenya Dkt. William Ruto amewataka wabunge wasibadilishe katika ya nchi hiyo kuhusu muda wa mihula miwili ambayo rais wa nchi hiyo anastahili kuwa madarakani.

Ruto amewataka wabunge wa chama chake cha United democratic Alliance kupuuzilia mbali mwito wa baadhi ya wabunge wa chama hicho kutaka katiba kufanyiwa marekebisho ili kumruhusu rais kuongoza bila ukomo.

Katiba ya Kenya inamruhusu rais kuwa madarakani kwa kipindi cha mihula miwili.

Kulingana na vyombo vya habari nchini Kenya wakenya wengi walikuwa na hamu ya kusikia msimamo wa raisi Ruto kuhusiana na kauli hiyo iliyotolewa wiki iliyopita.

Rais Ruto aliingia madarakani baada ya rais Kenyatta kumaliza mihula miwili madarakani inavyohitajika kikatiba. Aliapishwa kuwa rais mwezi Septemba mwaka huu.

Chama cha Ruto cha United Democratic Alliance - UDA, kilifanya mkutano wa wabunge wake ambapo aliwataka watilie mkazo sera ambazo zitaboresha maisha wa wakenya.

Amewataka kuachana na kile ametaja kama “ubinafsi”.

Baada ya kauli hiyo kuzua mzozo mkali katika chama kinachotawala cha UDA, huku mwenyekiti wa chama hicho Johnstone Muthama, akikanusha kuwepo kwa mipango ya kubadilisha katiba ili kumruhusu Ruto kuendelea kugombea Urais bila kikomo cha mhula.

XS
SM
MD
LG