Ulimwengu huzalisha takriban tani milioni 400 za uchafu wa plastiki kila mwaka, wakati chini ya asilimia 10 ya uchafu huo ukichakatwa ili kutumika tena, kulingana na program ya mazingira ya Umoja wa Mataifa.
Takriban tani milioni 14 za uchafu wa plastiki huishia baharini kila mwaka, Umoja wa Kimataifa wa Kulinda Mazingira umesema, wakati majalala ya taka taka yakiendelea kujaa.Wajumbe wa kimataifa wanakutana Kenya kwa duru ya tatu ya mazungumzo kuhusu hatua za kuchukuliwa kwenye mkataba huo.
Rais Ruto amewakumbusha waliohudhuria zimebaki wiki 6 pekee kuingia kwa mwaka 2024, na kuna mikutano miwili tu iliyobaki kuelekea kwenye mkataba huo.Serikali zilikubaliana Machi 2022 kwamba zingebuni mkataba wa kudhibiti tatizo la plastiki kufikia mwisho wa mwaka ujao.
Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayotaka sheria kali zipitishwe kuhusu utengenezaji na matumizi ya plastiki, wakati tayari ikiwa imepitisha sheria kadhaa za kupiga marufuku matumizi wa baadhi ya mifuko ya plastiki tangu 2017.
Ruto ameongeza kusema kwamba, “Ni lazima tubadili matumizi yetu ya plastiki, pamoja na namna ya kutupa taka hizo.”
Forum