Ruto ambaye alimteua aliyekuwa gavana wa benki kuu ya Kenya Prof Njuguna Ndung’u kuwa waziri wa fedha, amesema kwamba ataendelea kupunguza matumizi ya fedha mwaka ujao, kwa kiasi ambacho hakutaja mwaka.
Alikuwa akihutubia kikao cha bunge la taifa hii leo alhamisi.
Matumizi ya pesa za serikali ya Kenya yanahusu mishahara kwa watumishi wa serikali, malipo kwa huduma za ndani na nje ya nchi, gharama ya mafuta kwa magari ya serikali miongoni mwa mengine.
Kenya inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kutokana na mfumko wa bei, deni kubwa na ukame.
Amesema kwamba serikali haistahili kukopa pesa kwa ajili ya kulipa mishahara na gharama zingine, akisema kwamba ni lazima nchi irudi katika nidhamu ya kifedha.