Lavrov ameiambia RIA kwamba mahakama za nchini kwake zimewahukumu zaidi ya wawakilishi 200 wa jeshi la Ukraine, kwa kufanya unyama.
Pande zote zinashutumiana kwa kufanya unyama katika vita ambavyo vimeanzishwa na Russia baada ya kuivamia Ukraine, Febuari 2022. Umoja wa Mataifa unaendelea kupata ushahidi wa uhalifu wa kivita, na uvunjifu wa haki za binadamu uliofanywa na serekali ya Russia, ikijumuisha mateso, ubakaji, na usafirishaji wa watoto.
Mwezi Machi, mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Russia, Vladimir Putin, kwa usafirishaji wa watoto kuwa umefikia kiwango cha uhalifu wa kivita.
Forum