Rais wa Russia Vladimir Putin, Jumanne amesema Russia ipo tayari kuratibu shehena ya nafaka ya Ukraine kutoka bandari za Black Sea.
Lakini rais Putinanataka mataifa ya magharibi kuondoa vikwazo vyao dhidi ya usafirishwaji wa nafaka za Russia.
Rais Putin aliongea hayo baada ya mkutano na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, kuhusu mpango huo alopendekeza ili kuanza kwa usafirishaji wa shehena za Ukraine.
Uvamizi wa Russia umeleta taabu katika biashara za Ukraine, na kutokana na msukumo wa matatizo ya usambazaji chakula duniani, Umoja wa Mataifa umeshirikishwa katika mazungumzo ili kutoa zuiwo la usafirishaji wa chakula.
Farhan Haq, naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, aliwaambia wanahabari Jumanne matumaini ya Guterres ni kwamba makubaliano yatakamilika.
Aliongeza kusema kwamba katibu mkuu Guterres, aliongea na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu mazungumzo yanayo endelea.