Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:23

Russia yashambulia miji kadhaa ya Ukraine na kusababisha ukosefu wa umeme na maji


Idara ya wafanyakazi wazima moto yazima moto kwenye eneo la tukio baada ya shambulio la makombora ya Russia, nje ya mji mkuu Kyiv, Novemba 23, 2022. Picha ya AP
Idara ya wafanyakazi wazima moto yazima moto kwenye eneo la tukio baada ya shambulio la makombora ya Russia, nje ya mji mkuu Kyiv, Novemba 23, 2022. Picha ya AP

Miji kadhaa ya Ukraine ukiwemo mji mkuu wa Kyiv, imeshambuliwa mapema leo Ijumaa na msururu wa makombora ya Russia, maafisa wamesema, na kusababisha kukatika kwa maji na umeme katika maeneo mengi.

Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko amesema kwenye mitandao ya kijamii “ Kutokana na uharibifu wa miundombinu ya nishati, kuna tatizo la usambazaji wa maji katika maeneo yote ya mji mkuu.

Klitschko amesema milipuko ilitokea katika wilaya kadhaa za mji mkuu na kuwaonya wakazi kutoondoka kwenye makazi hayo, wakati mashambulizi yakiendelea.

Mji wa pili mkubwa wa Ukraine, Kharkiv nao umeripoti kukatika kwa umeme.

Meya wa mji huo Igor Therkov ameandika kwenye Telegram “ Kharkiv haina umeme.”

Katika tukio jingine, jengo la makazi katika mji wa kusini mwa Ukraine ,Kryvyi Rig, umeshambuliwa leo na kombora la Russia ambalo limeua watu wawili na kujeruhi wengine watano, gavana wa jimbo Valentyn Reznichenko amesema.

XS
SM
MD
LG