Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:14

Russia yashambulia miji kadhaa ya Ukraine kwa makombora na kuharibu miundombinu muhimu


Wafanyakazi wa zima moto wakijaribu kuzima moto baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye makazi mjini Kyiv, Oktoba 17, 2022. Picha ya AP
Wafanyakazi wa zima moto wakijaribu kuzima moto baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye makazi mjini Kyiv, Oktoba 17, 2022. Picha ya AP

Miji kadhaa ya Ukraine Alhamisi imeshambuliwa kwa makombora ya Russia na kuharibu vituo vya umeme na miundombinu mingine muhimu wakati huu wa msimu wa baridi kali.

Waziri mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal amesema vituo kadhaa vya nishati viliharibiwa na kwamba Russia inajaribu kuwanyima umeme wananchi wa Ukraine kabla ya mwaka mpya.

Hata hivyo, jeshi la Ukraine limesema limefaulu kudhibiti makombora mengi, na hivyo kuepusha uharibifu mkubwa.

“Kulingana na takwimu za awali, jumla ya makombora 69 yalirushwa. Makombora 58 ya adui yalitunguliwa,” mkuu wa jeshi la Ukraine, Jenerali Valeriy Zaluzhniy amesema.

Awali maafisa walisema zaidi ya makombora 120 yalirushwa, kwa mujibu wa Reuters.

Russia imekuwa ikitumia makombora mara kwa mara kulenga miji ya Ukraine, yakiwemo mashambulizi yaliyoharibu vituo vya miundombinu muhimu, licha ya kukanusha kuwa inawalenga raia.

XS
SM
MD
LG