Wizara ya Kilimo ya Ukraine ilithibitisha kuwa kulikuwa na nafaka zilizohifadhiwa bandarini wakati wa shambulio hilo, gazeti la Kyiv Independent liliripoti.
Nafaka hiyo ilitarajiwa kuuzwa nje ya nchi katika siku chache zijazo, kulingana na wizara hiyo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine ilisema kwamba "Russia itabeba jukumu kamili la kuzidisha mzozo wa chakula duniani" ikiwa makubaliano hayo yatasamaratika.
"Ilichukua chini ya saa 24 kwa Russia kufanya shambulio la kombora kwenye bandari ya Odesa, baada ya makubaliano hayo, ikivunja ahadi zake na kupuzilia makubaliano ya Istanbul kati ya Uturuki na Umoja wa Mataifa," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine Oleg Nikolenko alisema kupitia ujumbe wa Twitter.