Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:59

Russia yapata hasara kubwa Ukraine, kusajili raia wa kigeni kama wanajeshi


Watu wanaopiga picha wakiwa juu ya mizinga ya Russia iliyoharibiwa Kyiv, Ukraine. May 8, 2022
Watu wanaopiga picha wakiwa juu ya mizinga ya Russia iliyoharibiwa Kyiv, Ukraine. May 8, 2022

Bunge la Russia linatarajiwa kujadili mswada utakaoruhusu raia wenye umri wa zaidi ya miaka 40 na raia wa kigeni wanaoishi nchini humo wenye umri wa kuanzia miaka 30 kujiunga na jeshi.

Hatua hii ni ya Russia kuimarisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, baada ya kupoteza wanajeshi kadhaa katika vita vinavyoendelea.

Taarifa iliyoandikwa kwenye wavuti wa habari za serikali ya Russia, Duma, imesema kwamba hatua hiyo ni ya dharura, inayolenga kutumia ujuzi wa watu wazee wenye uwezo wa kivita.

Kwa sasa, wanajeshi wenye umri wa kati ya miaka 18 na 40 ndio wanaoruhusiwa kujiunga na jeshi la Russia.

Russia imepata pigo kubwa sana kwa kupoteza wanajeshi na silaha katika vita vya siku 86 sasa, ambapo Ukraine umefanikiwa kuwashawishi raia wake kupigana na kupinga uvamizi wa Russia.

Japo Russia imedhibithi Mariupol, imeshindwa kufikia malengo yake katika vita hivyo pamoja na kushindwa kudhibithi Donbas, mashariki mwa Ukraine.

Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu amesema kwamba Russia imeanda kuunda vikosi 12 vya jeshi katika sehemu za magharibi, kwa matayarisho ya kile ametaja kama vitisho vinavyoongezeka katika sehemu hiyo, akisema vinatokana na Finland na Sweden kuomba kuwa wanachama wa NATO.

XS
SM
MD
LG