Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 02:44

Russia yakabidhi kwa Kyiv maiti 210 za wapiganaji wa Ukraine


Wanajeshi wa Ukraine wakikaa ndani ya bus baada ya kuondolewa kwenye kiwanda cha chuma cha Azovstal cha mji uliozingirwa wa Mariupol, May 17, 2022. Picha ya AP
Wanajeshi wa Ukraine wakikaa ndani ya bus baada ya kuondolewa kwenye kiwanda cha chuma cha Azovstal cha mji uliozingirwa wa Mariupol, May 17, 2022. Picha ya AP

Russia imekabidhi kwa Kyiv maiti 210 za wapiganaji wa Ukraine, ambao wengi wao walifariki wakiulinda mji wa Mariupol usitekwe na wanajeshi wa Russia katika mapigano makali yaliyofanyika kwenye kiwanda kikubwa cha chuma, jeshi la Ukraine limesema Jumanne.

Raia wengi wa Ukraine walizuiliwa kwenye kiwanda cha chuma cha Azovstal kwa wiki kadhaa wakati Russia ikijaribu kuuteka mji huo wa Mariupol.

Wanajeshi wa Ukraine hatimaye walijisalimisha mwezi uliopita na kuwekwa mbaroni na Russia.

“Mchakato wa kurejesha maiti za wanajeshi waliofariki wakilinda Mariupol unaendelea. Kufikia sasa, maiti 210 za wanajeshi wetu zimerejeshwa, wengi wao ni walinzi mashuja wa Azovstal,” idara ya ujasusi ya wizara ya ulinzi ya Ukraine imesema kwenye Twitter.

Kumekuwa na habari chanya juu ya hatma ya walinzi wa kiwanda cha Azovstal wanaokadiriwa kuwa 2,000, Kyiv inataka wote wakabidhiwe katika ubadilishanaji wa wafungwa, lakini baadhi ya wabunge wa Russia wanataka baadhi ya wanajeshi wa Ukraine wafikishwe mahakamani.

“Kazi inaendelea kuwarejesha nyumbani walinzi wote wa Ukraine waliotekwa nyara,” idara hiyo ya ujasusi imesema.

Wiki iliyopita, ubadilishanaji wa maiti 160 kati ya Russia na Ukraine ulitangazwa na wizara ya Ukraine ya kuunganisha eneo lililokaliwa kwa muda.

XS
SM
MD
LG