Jeshi la anga la Ukraine, limesema mashambulizi hayo yalitumia makombora 37 kati ya 63, na ndege zisizo na rubani za Russia zilianzisha mashambulizi kote nchini humo, na malengo ya msingi yalikuwa ni miundombinu na maeneo ya kijeshi katika eneo la Odesa.
Bandari ya Odesa ilitumika kusafirisha nafaka chini ya makubaliano yaliyodumu kwa mwaka mmoja kabla ya Russia kutangaza kuyamaliza n kujitoa ushiriki wake mapema wiki hii.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, leo amesema kwamba mashambulizi ya sasa ya Russia, yalilenga miundombinu ya nafaka, na kila kombora la Russia lililipua sio tu Ukraine, bali kila mtu duniani ambaye anataka maisha ya kawaida na salama.
Forum