Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 21:10

Russia yadaiwa kuandikisha vifo vingi zaidi wiki zilizopita katika vita Ukraine


Wizara ya ulinzi ya Uingereza, Jumapili imesema kwamba katika  kipindi cha wiki mbili zilizopita, Russia, imekabiliwa na idadi kubwa ya vifo toka wiki ya kwanza ya uvamizi wake  nchini Ukraine takriban mwaka mmoja uliopita.

Uchunguzi wa wizara unatokana na taarifa za Ukraine kwamba Russia ilipata wastani wa vifo 824 kwa siku katika wiki iliyopita, ikiwa ni zaidi ya mara nne ya wastani ulioripotiwa mwezi Juni na Julai.

Wizara imesema takwimu hizo zinatokana na uwezekano wa kupata data sahihi kutoka Ukraine.

Kuongezeka kwa vifo vingi vya Russia, wizara imesema inawezekana inatokana na sababu kadhaa ikijumuisha ukosefu wa wapiganaji waliopata mafunzo, kutojipanga na rasilimai zinazohitajika mstari wa mbele.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG