Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 04:01

Russia yadai kushambuliwa na Ukraine


Maafisa wa Russia, Jumanne wamesema kwamba shambulizi la ndege zisizo na rubani za Ukraine lililenga bandari katika eneo la Krasnodar kusini mwa Russia, na kuua mtu mmoja na kujeruhi takriban wengine watano.

Shambulizi hilo lilipiga Port Kavkaz, Gavana wa Krasnodar, Veniamin Kondratyev, amesema kupitia mtandao wa Telegram.

Amesema moto ulizuka kwenye feri lakini ulidhibitiwa licha ya uharibifu wa kivuko kutoonekana mara moja.

Jeshi la Ukraine limesema shambulizi lake liliharibu kwa kiwango kikubwa kile ilichokiita feri ya reli. Bandari hiyo ipo katika ukanda wa ardhi kati ya Peninsula ya Crimea na Russia Bara.

“Watu hutumia feri hiyo kusafirisha mabehewa, magari, na makontena kwa matumizi ya kijeshi,” Mkuu wa Wafanyakazi wa Ukraine amesema kwenye mtandao wa kijamii.

Maelezo kutoka pande zote mbili Ukraine na Russia hayakuweza kuthibitishwa mara moja.

Forum

XS
SM
MD
LG