“Tutaona kama watafanya walivyoahidi,” Biden amesema baada ya kuzungumza kwa simu na viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Italia.
“Inaonekana kuna makubaliano lakini wacha tuone kile walichoahidi kufanya.”
Biden ametoa matamshi hayo kwa waandishi wa habari kwenye White House baada ya jeshi la Russia kusema mapema Jumanne kwenye duru ya mazungumzo ya hivi karibuni nchini Uturuki kwamba, litapunguza operesheni zake karibu na Kyiv na Chernihiv.
Naibu waziri wa ulinzi wa Russia Alexander Fomin amesema hatua hiyo ni kutaka kuongeza uaminifu katika mazungumzo yenye lengo la kumaliza mapigano.
Vikosi vya Russia vilikwama kusonga mbele hivi karibuni kufuatia kujihami vikali kwa wapiganaji wa Ukraine.
Jumanne pia, waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu amesema vikosi vya Russia vitajikita zaidi kwenye eneo la Donbas, ambalo linajumuisha majimbo yaliyojitenga ya Luhansk na Donetsk.