Moscow ilipendekeza mpango huo baada ya kuvunja mkataba ulioendelea kwa mwaka mmoja mwezi Julai, ambao uliiruhusu Ukraine kusafirisha nafaka kwa usalama kutoka bandari zake za bahari ya Black Sea, kwa matumaini ya kudhibiti kupanda kwa bei za vyakula duniani, kulikochochewa na uvamizi wa Russia.
Russia imekuwa ikizivutia nchi za Kiafrika, ambazo baadhi zimekuwa zikikabiliwa na uhaba wa chakula, kwa kuziahidi nafaka za bure au zilizopunguzwa bei - ingawa ni kiasi kidogo sana kuliko zile Ukraine imekuwa ikiuza nje.
"Makubaliano yote kimsingi yamefikiwa. Tunatarajia kwamba katika siku za usoni, tutaingia katika mawasiliano ya kufanya kazi, na pande zote, ili kushughulikia masuala yote ya kiufundi ya mpango kama huo," Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Alexander Grushko, aliwaambia waandishi wa habari, kwa mujibu wa shirika la habari la Russia, Interfax.
Kulingana na Moscow, Uturuki itashughulikia mauzo ya nje ya nafaka ya Russia lakini maelezo ya jukumu lake hayakuwa wazi.
Forum