Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 07:08

Russia: Raia wa Marekani ahukumiwa miaka minne jela kwa kumpiga teke afisa wa usalama


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Mahakama moja katika mji wa magharibi mwa Russia wa Voronezh Jumanne imemuhukumu raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 28 kifungo cha miaka minne na miezi sita jela, kwa kumpiga teke afisa wa usalama.

Kamati inayofanya uchunguzi kuhusu matukio makubwa ya uhalifu imesema katika taarifa , “ Mwanamme huyu ambaye alipinga hatua za kisheria zilizochukuliwa na mamlaka, alitumia vurugu dhidi ya afisa wa polisi aliyekuwa zamu na kumpiga mateke mara kadhaa.”

Mmarekani huyo aliyetajwa na shirika la habari la serikali ya Russia kama Robert Gilman, anakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, wakili wake amesema. Wakili Valery Ivannikov, ameongeza kuwa mteja wake anapanga kuwasiliana na maafisa wa Marekani ili kupanga ubadilishanaji wa wafungwa.

XS
SM
MD
LG