Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 00:59

Russia na Ukraine zajitolea vikosi katika miji ya Pavlivka na Vuhledar


Mabaki katika vita vya Russia na Ukraine

Wizara ya ulinzi ya uingereza imesema Russia na Ukraine zimejitolea vikosi vikubwa katika eneo kwenye miji ya Ukraine ya Pavlivka na Vuhledar huko kusini kati mwa Donetsk .

Wizara hiyo imesema katika taaarifa za kijasusi zilizochapishwa kwenye mtandao wa Twitter Jumapili, kwamba eneo hilo limeshuhudia mapambano makali katika wiki mbili zilizopita ingawa kuna eneo dogo lililobadilika.

Eneo hilo huenda likasalia kuwa linazozaniwa vikali , Wizara ya ulinzi iliongeza kusema kwa sababu Russia inatathmini kuwa eneo lina uwezo kufanyika uzinduzi wa maemndeleo makubwa ya siku zijazo huko kaskazini ili kukamata eneo lililobaki la Doneskk inayoshikiliwa na Ukraine.

Jumamosi Rais wa Ukraine Volodymir Zelenskyy aliandaa Mkutano wa kuadhimisha miaka 90 ya Holodomor au njaa kubwa , na kuendelea na mpango wa nafaka kutoka Ukraine na kupeleka nafaka katika nchi zilizzokumbwa zaidi ya njaa na ukame.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG