Rais wa Marekani, Barack Obama, kutokana na kujumuisho taarifa za upelelezi yanayoonyesha kuwa Russia ilihusika na juhudi za kuhujumu uchaguzi wa urais, amesema “hakuzipa uzito wa kutosha” athari ya kampeni za upotoshaji habari na uhalifu wa mitandao katika demokrasia.
Obama akiwa amebakiza siku 12 kumaliza muda wake amekiambia kituo cha televisheni cha ABC News (wiki hii) kwamba hafikiri kama alidharau uwezo wa rais wa Russia, Vladimir Putin katika uhalifu huu, ambao umedaiwa na idara za kipelelezi za Marekani, kwa kuamuru kwake juhudi hizo za kuvuruga mifumo ya uchaguzi wa kidemokrasia Marekani.
Pia aliongeza kusema katika hilo kuhusika kwake Putin katika kufanya hasimu wa kisiasa wa rais mteule Donald Trump, Hillary Clinton wa Demokratik kushindwa.
Lakini Obama amesema, “ Nafikiri nilikuwa nimekadiria vibaya kiwango ambacho, katika zama hizi za teknolojia ya habari mpya, ni rahisi kwa taarifa potofu kupenyezwa kwenye mitandao na mengineyo, kuwa na athari katika jamii zetu zilizokuwa na uwazi, mifumo yetu inayofikiwa, kuwa ilikuwa inawezekana maadui zetu kujipenyeza katika harakati zetu za kidemokrasia katika njia ambazo nafikiri zinaonekana kutia kasi.”
Amesema kuwa aliamuru kutoa muhtasari wa taarifa za kipelelezi juu ya uhalifu wa mitandao uliofanywa na Russia “ ili kuhakikisha tunafahamu hili ni jambo ambalo Putin amekuwa akilifanya kwa muda mrefu hivi sasa huko ulaya, mwanzoni katika yaliyokuwa majimbo katika himaya ya Umoja wa Sovieti ambako kuna watu wengi wanaozungumza kirusi, lakini hivi leo uingiliaji wake huo umezidi katika demokrasia ya nchi za Magharibi.
Hivi karibuni taarifa za kipelelezi zilifanya majumuisho na kutoa muhtasari wao kuwa rais wa Russia, Vladimir Putin alikusudia kuvuruga uchaguzi wa Marekani wa 2016 na kumchafua aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekan, Hillary Clinton katika “kampeni chafu” ambayo haijawahi kutokea.
Hatimaye rais huyo aliamua kumsaidia rais mteule, Donald Trump, imesema taarifa ya ripoti iliyoidhinishwa kutumika kwa umma na idara za vyombo vya upelelezi vya Marekani, taarifa hiyo ilieleza.
Pia ilisema dhamiri ya Russia ilikuwa kufanya umma upoteze imani katika mchakato wa demokrasia ya Marekani, kumdhalilisha waziri Clinton, na kuchafua nafasi yake ya kuchaguliwa,” kwa mujibu wa hiyo taarifa iliyotolewa baadae Ijumaa.