Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 16:33

Russia kuongeza mashambulizi wiki hii, Zelenskyy adai


Mkazi wa Ukraine nje ya nyumba iliyoharibiwa na mashambulizi
Mkazi wa Ukraine nje ya nyumba iliyoharibiwa na mashambulizi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema Jumatatu kwamba tutarajie kuwepo mashambulizi makali kutoka Russia wiki hii, wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wanapo tathmini iwapo waunge mkono kuikubali Ukraine kuomba kujiunga na muungano huo.

Katika hotuba yake Jumapili usiku, Zelenskyy amesema kwamba huu ni wakati muhimu kwa maamuzi katika historia ya Ukraine. Ameongeza kusema kwamba mapigano makali yanaendea Donbas, mkoa wa mashariki mwa taifa hilo ambako Russia imekuwa ikililenga katika miezi ya karibuni.

Tume ya EU wiki iliopita ilipendekeza kwamba Ukraine inaweza kupewa hadhi kuwa mgombea wa kuomba uanachama wa EU. Mataifa 27 ya muungano huo yanatarajiwa kupiga kura kuhusiana na suala hilo kwenye kikao cha Alhamisi na Ijumaa. Iwapo Ukraine itakubaliwa kuomba kujinga na EU, basi mchakato wa kujiunga huenda ukachukua miaka kadhaa.

XS
SM
MD
LG