Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:04

Russia ipo tayari kufanya mazungumzo na Ukraine


Rais wa Russia Vladimir Putin akiongoza mkutano wa viongozi wa viwanda vya kijeshi mjini Tula, Russia. Dec. 23, 2022.
Rais wa Russia Vladimir Putin akiongoza mkutano wa viongozi wa viwanda vya kijeshi mjini Tula, Russia. Dec. 23, 2022.

Rais wa Russia Vladimir Putin, amesema kwamba nchi yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Ukraine, kuhusu maswala yanayoweza kufikia makubaliano.

Putin amesema hayo katika mahojiano ya televisheni ya taifa.

Amesema kwamba sio kweli kwamba Russia ndio imekataa kufanya mazungumzo, bali ni Ukraine.

Putin amesema kwamba Moscow haina uwamuzi mwingine, na kwamba anaamimi kuwa Kremlin inachukua hatua zinazofaa.

Ameongezea kwamba anatetea maslahi ya kitaifa, ya raia na watu wake.

Amesisitiza kwamba hana uwamuzi mwingine wa kufanya kando na kulinda watu wa Russia, lakini yupo tayari kufanya mazungumzo ambayo matokeo yake yatakubaliwa na wahusika wote katika mazungumzo hayo.

XS
SM
MD
LG