Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:47

Russia inataka vikwazo dhidi yake kuondolewa katika mazungumzo ya kusafirisha nafaka


Meli ya Despina V, ikiwa imebeba nafaka ya Ukraine ikipita black sea, karibu na Istanbul, Uturuki, Uturuki, Nov 2, 2022
Meli ya Despina V, ikiwa imebeba nafaka ya Ukraine ikipita black sea, karibu na Istanbul, Uturuki, Uturuki, Nov 2, 2022

Rais wa Uturuki Recp Tayip Erdogan, amefanya mazungumzo na viongozi wa Russia na Ukraine kuhusu usafirishaji wa nafaka kupitia bahari ya Black Sea, huku pande zote zikitafuta mabadiliko yatakayopelekea kuongeza kiwango cha nafaka kinachosafirishwa kutoka nchini mwao.

Uturuki na Umoja wa Mataifa wamekuwa wapatanishi katika kutafuta maelewano kuhusu usafirishaji wa nafaka, ambao ulipelekea kusafirishwa kwa nafaka kutoka bandari za Ukraine, miezi sita baada ya Russia kuzuia usafirishaji huo.

Russia inatafuta kuwa na uwezo mkubwa wa kuuza chakula na mbolea kutoka nchini mwake, huku Ukraine ikitaka makubaliano hayo kupanuliwa na kuruhusu bandari zake kadhaa kufunguliwa kwa usafirishaji.

Ofisi ya rais wa Uturuki imesema kwamba rais wa Uturuki Recep Tayip Erdogan ametoa wito wa kumalizwa haraka kwa vita nchini Ukraine na kwamba utawala wa Moscow unaweza kuanza kuuza kiasi kikubwa cha chakula na bidhaa nyingine kupitia bahari ya Black Sea.

Russia inaitaka Umoja wa Mataifa kuzishinkiza nchi za magharibi kuondoa vikwazo vya uchumi dhidi yake ili iwe na uwezo wa kusafirisha mbolea na chakula bila vizuizi.

XS
SM
MD
LG