Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 03:44

Russia inataka kujua nchi zinazonunua nafaka kutoka Ukraine


Meli iliyokodishwa na umoja wa mataifa ikiwa imebeba tani 30,000 za nafaka kutoka Ukraine ikiwasili katika bandari ya Djibouti. Nafaka hiyo ilikuwa inaelekea Ethiopia. Augn 30, 2022
Meli iliyokodishwa na umoja wa mataifa ikiwa imebeba tani 30,000 za nafaka kutoka Ukraine ikiwasili katika bandari ya Djibouti. Nafaka hiyo ilikuwa inaelekea Ethiopia. Augn 30, 2022

Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov amesema kwamba Moscow imeomba umoja wa Mataifa kutoa ripoti kamili kuhusu kiasi na mahali nafaka kutoka Ukraine inapelekwa.

Russia imesema kwamba utoaji wa ripoti hiyo ndiyo itapelekea maamuzi kuhusu mkataba wa kuongeza muda kwa usafirishaji wa nafaka kutoka bandari za black sea hadi masoko ya kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lavrov amesema kwamba hoya ya Russia sio tu ya kuonyesha kutokuwa na Imani na kwamba mkataba wa kuruhusu usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine utategemea ripoti hiyo.

"Nasisitiza kwamba nchi zinazonufaika na usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kufuatia mkataba wa Istanbul wa July 22, zio mojawapo ya nchi maskini duniani. Nchi maskini zinapokea kiasi kidogo sana cha nafaka hiyo kutoka Ukraine kutoka Black Sea. Zaidi ya nusu ya nafaka kutoka Ukraine inaingia katika umoja wa Ulaya na kuna ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu kiasi kinachosafirishwa,” amesema Lavrov.

Russia ilisaini mkataba wa kusafirisha nafaka kutoka Ukraine mnamo mwezi July, uliosimamia na Uturuki.

Russia ilikuwa imezuia usafirishaji wa nafaka hiyo tangu ilipovamia Ukraine kijeshi, ambao imesema ni oparesheni maalum.

Russia imesema kwamba nafaka hiyo haifiki katika nchi maskini zaidi duniani na kuonyesha dalili za kutokuwa tayari kuongeza mda zaidi wa mkataba huo.

XS
SM
MD
LG