Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 14:08

Russia inasema haijachukua uamuzi wa mwisho kuruhusu tena usafirishaji wa nafaka ya Ukraine


Nafaka iliyohifadhiwa katika bandari ya Ukraine ya Izmail, Aprili 26, 2023.
Nafaka iliyohifadhiwa katika bandari ya Ukraine ya Izmail, Aprili 26, 2023.

Russia Jumatano imesema kwamba bado haijachukua uamuzi wa mwisho kuhusu kuongeza muda wa makubaliano ya kusafirisha nafaka kutoka bandari ya Black Sea ambayo muda wake unatarajiwa kumalizika tarehe 17 Julai.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewambia waandishi wa habari kwamba hakuna uamuzi rasmi uliotangazwa bado kuhusu kuongeza muda wa makubaliano hayo, ambayo yanaruhusu usafirishaji salama wa nafaka kutoka Ukraine.

Russia ilisema mara kwa mara kuwa haioni sababu za kuongeza muda wa makubaliano hayo baada ya Julai 17 kwa sababu ya vikwazo kwa mauzo yake ya nafaka na mbolea.

Lakini Peskov amesema muda bado upo kwa nchi za magharibi kushugulikia masuala hayo.

Chini ya makubaliano hayo, Russia ilihakikisha usalama kwa meli zinazozafirisha nafaka kuelekea na kutoka kwenye bandari za Ukraine zilizo chini ya udhibiti wake.

Forum

XS
SM
MD
LG