Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:23

Russia inadai kuua wanajeshi 600 wa Ukraine lakini hakuna uharibifu wala damu kwenye kambi iliyolengwa


Sehemu iliyopigwa na kombora la Russia, Kramatorsk, Ukraine Jan 8, 2023
Sehemu iliyopigwa na kombora la Russia, Kramatorsk, Ukraine Jan 8, 2023

Shambulizi la Russia katika mji wa Kramatorsk nchini Ukraine limekosa kupiga sehemu iliyokuwa imelengwa na hakuna dalili yoyote ya kwamba vifo vilitokea.

Russia imedai kwamba shambulizi hilo limesababisha vifo vya wanajeshi 600 wa Ukraine, lakini mwandishi wa shirika la habari la Reuters aliyefika sehemu hiyo amesema kwamba hakuna ishara ya kutokea kifo.

Waandishi wa shirika la habari la Reuters wametembeela sehemu ambayo Russia imedai kwamba imeharibu kambi ya wanajeshi wa Ukraine, na ambayo kombora lilikuwa limelenga.

Hakuna uharibifu umetokea kwenye kambi hiyo iliyo mashariki mwa mji wa Kramatorsk. Hakuna tone la damu limeonekana.

Kombora la Russia lilikuwa la kulipiza kisasi baada ya shambulizi la Ukraine la mkesha wa mwaka mpya, lililosababisha vifo kadhaa vya wanajeshi wa Russia.

Msemaji wa jeshi la Ukraine katika sehemu za mashariki mwa nchi Serhiy Cherevatyi, ametaja madai ya Russia kwamba wameua wanajeshi 600 wa Ukraine kuwa uongo wa kujaribu kudai kwamba imejibu shambulizi baya la hivi karibuni la Ukraine dhidi ya wanajeshi wa Russia.

XS
SM
MD
LG