Ulinzi wa anga wa Russia ulitungua zaidi ya ndege 100 zisizo na rubani za Ukraine leo Jumapili katika mikoa ya magharibi mwa Russia, maafisa wa Moscow wamesema huku watu 17 walijeruhiwa katika mji wa Ukraine wa Kryvyi Rih katika shambulio la kombora la masafa marefu.
Wizara ya ulinzi ya Russia imesema ndege zisizokuwa na rubani 110 ziliharibiwa katika mashambulizi ya usiku kucha dhidi ya mikoa saba ya Russia. Mashambulio mengi yalilenga mkoa wa mpakani wa Russia wa Kursk, ambako ndege 43 zisizo na rubani ziliripotiwa kutunguliwa.
Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionekana kuonyesha ulinzi wa anga ukiwa kazini katika mji wa Dzerzhinsk katika mkoa wa Nizhny Novgorod, karibu na kiwanda kinachotengeneza vilipuzi. Gavana wa mkoa huo Gleb Nikitin aliandika kwenye mitandao ya kijamii leo Jumapili kwamba wafanyakazi wanne wa zima moto wamejeruhiwa wakati wakizima shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani katika eneo la viwanda la Dzerzhinsk, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Forum