Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 14:05

Russia imetishia kuharibu satelaiti za Marekani


Roketi ya Russia aina ya Sayuz ikiwa imebeba satellite, ikipaa kwenda angani kutoka Vostochny, nje ya mji wa Tsiolkovsky, kilomita 200 kutoka mji wa Blagoveshchensk mashariki mwa Russia, Nov. 28, 2017.
Roketi ya Russia aina ya Sayuz ikiwa imebeba satellite, ikipaa kwenda angani kutoka Vostochny, nje ya mji wa Tsiolkovsky, kilomita 200 kutoka mji wa Blagoveshchensk mashariki mwa Russia, Nov. 28, 2017.

Afisa wa ngazi ya juu katika wizara ya mambo ya nje ya Russia amesema kwamba vifaa vya satelaiti vya Marekani na washirika wake vinaweza kulengwa na Russia iwapo watajihusisha na vita nchini Ukraine.

Russia, ambayo ilizindua satelaiti yake ya kwanza mwaka 1957, na kutuma binadamu wa kwanza kwenda anga za juu mwaka 1961, ina uwezo mkubwa wa kivita katika anga za juu, namna ilivyo na Marekani pamoja na China.

Mnamo mwaka 2021, Russia ilizindua makombora yake ya satelaiti na kuyatumia kuharibu mojawapo ya satelaiti zake.

Naibu mkurugenzi anayesimamia maswala ya silaha katika wizara ya mambo ya nje ya Russia Konstantin Vorontsov, ameuambua Umoja wa Mataifa kwamba Marekani na washirika wake wanajaribu kutumia anga za juu kueneza ubabe wa nchi za Magharibi.

Vorontsov amesema kwamba kutumia mitambo ya satelaiti ya nchi za Magharibi kusaidia katika vita vya Ukraine ni mwenendo hatari sana na kwamba hatua ya mataifa ya Magharibi kutumia mitambo hiyo kuisaidia Ukraine ni ya uchokozi.

Hakuitaja kampuni yoyote ya satelaiti japo kampuni ya Elon Musk ilisema mapema mwezi huu kwamba kampuni yake itaendelea kufadhili huduma za internet nchini Ukraine, kwa ajili ya kutimiza kile alichokitaja kama matendo mema.

XS
SM
MD
LG