Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 10:51

Russia imeripoti uharibifu kwa ndege zisizo na rubani za Ukraine


Mfano wa ndege zisizotumia rubani yaani Drone.
Mfano wa ndege zisizotumia rubani yaani Drone.

Wakati huo huo mashambulizi ya anga ya jeshi la Ukraine siku ya Jumanne yaliulenga mji mkuu wa Russia

Maafisa wa Russia waliripoti uharibifu leo Jumanne kwa ndege zisizo na rubani za Ukraine zilizofanya mashambulizi katika maeneo mawili ya mafuta nchini Russia, huku pia wakisema vikosi vya Russia vilizima jaribio la mashambulizi ya ardhini ya kuvuka mpaka yaliyofanywa na wanamgambo wanaoiunga mkono Ukraine.

Makundi mawili ambayo yanadai kuwa yanaundwa na Wa-Russia wanaoipinga Kremlin yamesema yalivuka mpaka na kuingia Russia. Wizara ya ulinzi ya Russia imesema kuwa makundi ya kigaidi ya Ukraine yalijaribu kuivamia Russia kutoka pande tatu, ikiwemo kuyalenga mikoa ya Belgorod na Kursk.

Mashambulizi ya anga ya jeshi la Ukraine siku ya Jumanne yaliulenga mji mkuu wa Russia, pamoja na mikoa inayopakana na Ukraine na kuingia ndani zaidi katika eneo la Russia. Gavana wa mkoa wa Nizhny Novgorod, uliopo takriban kilomita 775 kutoka Ukraine, alisema ndege isiyo na rubani ya Ukraine ilichoma moto kiwanda cha kusafisha mafuta.

Forum

XS
SM
MD
LG