Russia imefanya operesheni za kupambana na ugaidi katika mkoa wa kusini wa Dagestan leo Jumapili, na kuwatia mbaroni watu watatu, Kamati ya Taifa ya Dhidi ya Ugaidi imesema.
Russia iko katika hali ya tahadhari ya kiwango cha juu kufuatia shambulizi la risasi la halaiki kwenye ukumbi wa tamasha mjini Moscow Machi 22, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka 20 ambapo watu wasiopungua 144 waliuawa.
Idara za usalama ziliwakamata majambazi watatu ambao walikuwa wakipanga matukio kadhaa ya kigaidi. Wakati wa ukaguzi wa maeneo ambayo wahalifu hao walikamatwa, zilipatikana bunduki za rashasha, risasi, na vifaa vya milipuko ambavyo vilikuwa tayari kutumiwa, kamati hiyo ilisema Jumapili.
Awali, kamati hiyo ilisema washukiwa wa uhalifu walizuiliwa na idara za usalama katika nyumba kadhaa kwenye maeneo ya makazi ya mji mkuu wa mkoa Makhachkala na moja ya miji mikubwa sana katika jamhuri, Kaspiysk.
Forum