Maafisa wa Ukraine wamesema kwamba wanajeshi wa Ukraine wamepiga na kuangusha makombora 16 kati ya 36 yaliyorushwa na Russia.
Mashambulizi hayo ya Russia yametokea wakati Norway imeidhinisha msaada wa kiasi cha dola bilioni 7 kwa Ukraine.
Rais wa Ukriane Volodymyr Zelenskyy amesema kwamba hatua hiyo inaimarisha sana uhusiano kati ya Norway na Ukraine, na kwamba Russia haitavuruga umoja wa nchi zinazotambua uhuru wao.
Maafisa wa Ukraine wameonya kwamba huenda Russia ikaanzisha mashambulizi mapya, wakati inatimia mwaka mmoja tangu ilipoivamia Ukraine.
Zelenskyy amesema kwamba ana imani kwamba Ukraine itashinda nguvu jaribio la Russia kutaka kunyakua kimabavu sehemu za Ukraine.
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kukutana kuijadili Russia
Rasimu ya makubaliano ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa, inayotarajiwa kupigiwa kura wiki ijayo, inataka vita vya Ukraine kumalizika mara moja, na makubaliano ya amani kupatikana yanayohakikisha kwamba uhuru wa Ukraine, umoja na mipaka yake unaheshimiwa.
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuidhinisha makubaliano hayo katika kikao kitakachofanyika Februari 23, siku moja kabla ya kutimia mwaka mmoja tangu Russia ilipoivamia Ukraine kijeshi.
Rasimu hiyo inataka Umoja wa Mataifa na nchi wanachama kuunga mkono juhudi za kidiplomasia ili amani ipatikane.
Wanaitaka Russia kuacha kushambulia mifumo muhimu ya Ukraine na kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini Ukraine.
Makubaliano ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa hayalindwi kisheria, lakini yana nguvu kubwa kisiasa.
Facebook Forum