Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:23

Russia imeendelea kuharibu mifumo ya nshati ya Ukraine kwa makombora


Miji kadhaa ya Ukraine imekosa umeme baada ya Russia kuharibu mifumo ya umeme Oct 31, 2022
Miji kadhaa ya Ukraine imekosa umeme baada ya Russia kuharibu mifumo ya umeme Oct 31, 2022

Wanajeshi wa Russia wamelenga mifumo ya nishati ya Ukraine kwa makombora katika mfululizo wa mashambulizi mapya ambayo maafisa wa Ukraine wameyataja kuwa ugaidi.

Milipuko imesikika katika sehemu kadhaa za nchi hiyo, ikiwemo katika bandari ya kusini ya Odesa, mji mkuu wa Kyiv, mji wa Dnipro na mkoa wa kusini mashariki wa Zaporizhzhia ambapo maafisa wamesema kwamba watu wawili wameuawa.

Waziri mkuu Denys Shmyhal, amesema kwamba makombora ya Russia yamelenga kiwanda kikubwa cha ulinzi cha Pivdenmash huko Dnipro, japo hajatoa maelezo zaidi kuhusu uharibifu uliotokea.

Kampuni ya nishati ya Naftogaz, inayomilikiwa na serikali imesema kwamba mitambo yake ya kutengeneza gesi imeharibiwa kutokana na mashambulizi ya makombora kadhaa.

XS
SM
MD
LG