Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 06:59

Rubani wa Ukraine aanza kunywa vimiminika baada ya mgomo


Rubani wa Ukraine, Nadiya Savchenko.
Rubani wa Ukraine, Nadiya Savchenko.

Rubani wa Ukraine, Nadiya Savchenko, ameanza kunywa vimiminika kwa mujibu wa mwanasheria wake.

Rubani wa Ukraine, Nadiya Savchenko, ambaye alikuwa katika mgomo wa kula toka wiki iliyopita kupinga mashitaka ya jinai ya Russia dhidi yake ameanza kunywa vimiminika kwa mujibu wa mwanasheria wake.

Nikolai Polozov alichapisha ujumbe kupitia Twitter leo hii kwamba mteja wake amemaliza mgomo wake wa kutokulwa ikiwa ni siku moja baada ya kufika mahakamani kukabiliana na mashitaka yake ya mauaji ya wanahabari wawili wa Russia mwaka 2014 kwa shambulizi katika mji wa Ukraine wa eneo Luhansk.

Hapo jana wakati Savchenko alipofikishwa katika mahakama ya Russia kukabiliana na mashitaka, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko aliweka video kupitia mitandao ya kijamii na kuiita kesi ya Savchenko ya “vichekesho” inayofanyika katika mahakama ya batili.

XS
SM
MD
LG