Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 12:27

Iran yamchagua tena Rais Rouhani


Mwanamke wa Kiiran wakati wa kampeni
Mwanamke wa Kiiran wakati wa kampeni

Rais wa Iran aliyekuwa anatetea kiti chake kwa mhula wa pili ametangazwa mshindi kwa asilimia 58.6.

Katika uchaguzi uliofanyika jana Ijumaa, Hassan Rouhani alimshinda mpinzani wake wa karibu Ebrahim Raisi aliyepata asilimia 39.8.

Ebrahim Raisi anayeungwa mkono na Kiongozi wa Kidini wa nchi hiyo Ayatollah Ali Khamenei, ni mmoja wa viongozi wa kidini mwenye msimamo mkali dhidi ya sera za mataifa ya magharibi.

Uchaguzi huo ulikuwa jaribio kubwa kwa Rais Rouhani kufuatia sera zake za mageuzi ambapo ameifanya Iran kuwa karibu na mataifa ya magharibi, na kuweza kuingia mkataba na mataifa yenye nguvu juu ya mradi wake wa nyuklia.

XS
SM
MD
LG