Gavana wa zamani wa jimbo la Massachusetts, Mitt Romney ameshinda kwenye uchaguzi wa awali maarufu kama “Super Tuesday” katika jimbo muhimu la Ohio, lakini ulikuwa ni ushindi uliopishana kwa kura chache dhidi ya seneta wa zamani wa Pennyslvania, Rick Santorum ambaye bado anaendelea na kampeni za uchaguzi wa awali katika kinyan’ganyiro cha uteuzi wa kuwania urais kupitia chama cha Repuplican.
Ulikuwa ni usiku mzuri kwa Mitt Romney. Alishinda wajumbe wengi katika majimbo 10 ambayo yalifanya uchaguzi wa awali wa kumteuwa mgombea wa nafasi ya kiti cha rais, ikiwemo jimbo la Ohio ambapo ushindi wa kura chache alioupata dhidi ya Rick Santorum haukuweza kutangazwa mara moja hadi majira ya saa sita usiku kwa saa za Ohio.
Mmoja wa wapiga kura wa Romney alisema “nimempigia kura Mitt Romney kwa sababu nadhani ni mtu shupavu, na ninataka tukio hili liishe ili tuweza kuanza kulenga namna ya kumshinda Rais Barack Obama.”
Casey Welch alimpigia kura Romney na alisema “nimempigia kura Mitt Romney leo. Ninafikiri ni mtu anayefaa kuurejesha uchumi kwenye njia sahihi na kuwasaidia wamarekani kusonga mbele.”
Wapiga kura wengi wa Repuplican bado hawana uhakika. Romney anaongoza lakini sio mgombea ambaye tayari anaelekea kupata uteuzi. Baadhi ya wapiga kura wanahisi waconservative kama Santorum na Newt Gingrich, ambaye alishinda kwenye jimbo alilozaliwa la Georgia, wamegawanyika.
Uchumi ni suala muhimu na wapiga kura huko Ohio na miji mingine wanakhofu kuhusu kupoteza ajira na kupanda kwa deni la taifa. Na kuna baadhi ya wa-Repuplican wa muda mrefu wana mpango wa kumpigia kura mdemocract, Rais Barack Obama.
Ulikuwa ni usiku mzuri kwa Romney, lakini sio mgombea ambaye tayari anaelekea kupata uteuzi. Santorum bado anaendelea na kampeni zake