Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:36

Romney atarajia ushindi Illinois


Wagombea nafasi ya kiti cha rais kwa chama cha Repuplican nchini Marekani
Wagombea nafasi ya kiti cha rais kwa chama cha Repuplican nchini Marekani

Mitt Romney bado anaongoza katika uchaguzi wa awali akiwa na wajumbe 521 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Santorum

Mgombea kiti cha rais kupitia chama cha Repuplican, Mitt Romney, anamatumaini ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa awali wa chama hicho utakaofanyika Jumanne katika jimbo la kati la Illinois, huku akitafuta kuongeza ushindi wake dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Rick Santorum.

Uchunguzi wa maoni unaonesha Romney ana ongoza kwa asilimia 15 mbele ya Santorum huko Illinois. Katika uchaguzi huo kuna wajumbe 69 wanaopiganiwa katika jimbo hilo na iwapo Romney atashinda, basi atapata nguvu nyingi ya kusonga mbele katika matukio yajayo ya kuteuliwa mgombea wa chama. Gavana huyo wa zamani wa Massachusetts tayari ameshashinda wajumbe 521, huku Santorum ameshinda wajumbe 253.

Wagombea wengine wawili wa Repuplican, Newt Gingrich na Ron Paul wapo nyuma kabisa. Jumatatu Romney na Santoru walifanya kampeni zao za mwisho mwisho katika jimbo la Illinois. Romney alikutana na wapiga kura kwenye chakula cha jioni katika mji mkuu, Springfield, kabla ya kuelekea Chicago kuhutubia suala la uchumi. Aliahidi kudhibiti matumizi ya serikali. “Ninataka kurejesha kanuni ambazo zimeifanya Marekani kuwa taifa kubwa duniani na moja ya kanuni hizo ni kutotumia zaidi ya unachopokea.”

Santorum anasema kwamba kama anashinda katika uchaguzi wa awali wa Jumanne, atakuwa mgombea wa kiti cha rais kupitia chama cha Repuplican. Seneta huyo wa zamani aliwasihi wafuasi wake wawashawishi wapiga kura wengine wajitokeza kumpigia kura yeye. “Huu unaweza kuwa muda wa kipekee katika historia ya Marekani na hasa hapa Illinois unaweza kutekeleza hilo. Unaweza kuwashangaza wengine, wapigie kura wahafidhina.”

Jumapili Romney alishinda wajumbe 20 katika uchaguzi wa awali wa Puerto Rico na kumsogeza mbele kufikia wajumbe 1,144 waliohitajika ili kupata ushindi wa uteuzi wa chama cha Repuplican katika kinyang’anyiro cha nafasi ya kiti cha rais. Mshindi atakabiliana na Rais Barack Obama katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.

XS
SM
MD
LG