Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:02

Roboti ya kwanza kuwa mwanafunzi chuo kikuu Duniani


Roboti Bina48
Roboti Bina48

Jaribu kufikiria kuwa wewe ni mwanafunzi wa chuo kikuu huko Notre Dame de Namur katika mji wa Belmont, jimbo la California nchini Marekani.

Unaingia katika kipindi cha falsafa siku ya kwanza ya muhula mpya na kukutana na robot akikuelekea mkabala wa macho yako.

Roboti ni kifaa cha kielektroniki chenye uwezo wa kimekanika. Lakini roboti huyu sio ni kipande cha mashine kubwa ambacho kinatengeneza magari, au ni kifaa kidogo kinacho safisha sakafu. Huyu ni mfano wa binadamu aliyewahi kuishi akiitwa Bina48.

Bina48 anafanana na mwanadamu- angalau kichwa na mabega yake. Sauti yake inafanana kama ya mwanadamu. Na mnamo msimu wa baridi kuanza mwaka 2017, amekuwa ni roboti wa kwanza kabisa aliyekuwa na akili ya bandia iliyomwezesha kukamilisha kipindi cha mafunzo katika chuo kikuu.

Ni nani Bina48

Bina48, ni roboti au mashine ya kwanza kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu ulimwenguni.

Hadithi ya Bina48 ilianza miaka 13 iliyopita. Mnamo mwaka 2004, mfanyabiashara mwanamke Martine Rothblatt alianza kutafiti juu ya uwezekano wa kutumia teknolojia kuweza kuendeleza akili ya mwanadamu baada ya mtu kiwiliwili chake kufa.

Jumuiya ya Rothblatt, ambayo inajulikana kama Taasisi ya Movement Foundation, ilitengeneza mfumo wa kuhifadhi mawazo, maoni na kumbukumbu za binadamu katika kompyuta. Taasisi hiyo inaziita kumbukumbu hizi ni “mafaili ya akili.”

Katika mwaka 2007, taasisi hiyo iliitaka kampuni ya roboti ya Hanson Robotics kutengeneza programu ya akili ya bandia (A.I) ikitumia Mafaili ya akili.

Programu hiyo imekuja kuwa inawakilisha mwanadamu aliyeishi kwa kutumia teknolojia ya roboti. Mtu aliyechaguliwa na wataalamu wa kutengeneza roboti alikuwa mke wa Rothblatt ambaye ni Bina Aspen Rothblatt.

Bruce Duncan ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Terasem Movement Foundation anasema kuwa programu iliyomtengeneza Bina48 inahusisha sehemu kubwa ya mawazo, maoni na kumbukumbu zake zilizokuwa zimehifadhiwa kabla ya kufa. Duncan anasema kuwa roboti huyo anauwezo wa kutumia kumbukumbu hizi kwa njia ya kipekee kutengeneza habari mpya na kusema kama anavyozungumza mwanadamu.

Lakini akili za roboti huyu hazifanyi kazi sawa na vile za mwanadamu. Na roboti huyu hana uwezo wa kufikia umahiri wa hali ya juu wa akili ya bandia iliyoweza kutengenezwa na teknolojia iliyopo sokoni. Pia Duncan anatetea kuwa Bina48 anaweza kueleza kwa kiasi fulani ufahamu wake wa mazingira ambayo yanamzunguka.

XS
SM
MD
LG