Barua kutoka kwa kwa Kim Jong Un, iliyoelezea nia yake ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, iliwasilishwa na dadake kiongozi huyo, Kim Yo Jong, wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa heshima ya timu ya Korea Kaskazini kwenye ikulu ya Korea Kusini, Blue House.
Msemaji wa rais wa Korea Kusini, Kim Eui-Kyeom, alisema kuwa dadake Kim Jong Un aidha aliongeza kwamba rais Moon anakaribishwa kutembea Pyongyang wakati wowote akiwa tayari.
Rais Moon alielezea nia yake ya kufanya ziara hiyo, baada ya kuweka mikakati ifaayo katika siku za usoni.
Wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo siku ya Ijumaa, rais Moon aliwapa mkono wajumbe wa Korea Kaskazini na umati ukashangilia kwa shangwe na vigelegele katika kile kilichoonekana kama ishara ya uimarishaji wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ambazo zimekuwa na uhasimu wa muda mrefu.