Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:04

Warepublican wakutana Cleveland


Maelfu ya wanachama na wajumbe wa chama cha Republican nchini Marekani wanakusanyika katika mji wa Cleveland, Ohio, katika mkutano mkuu wa uteuzi wa chama hicho ambapo watamteua rasmi bilionea Donald Trump kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.

Mkutano huo unaanza Jumatatu utaendelea kwa siku nne kama kilele cha uchaguzi wa awali uliokuwa unaendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja, kuanzia wagombea zaidi ya 17 na hatimaye Trump kuibuka akiwa amebaki kileleni peke yake ulipoingia mwezi Mei 2016.

Cleveland katika takwimu:

  • Idadi ya wajumbe: 2,472
  • Wajumbe Mbadala: 2,302
  • Idadi ya wajumbe inayohitajika kushinda uteuzi wa chama: 1,237
  • Makisio ya waandishi wa habari: 15,000
  • Watu wanaotazamiwa kutembelea Cleveland wakati wa mkutano: 50,000
  • Makisio ya gharama za mkutano huo: $60 million
  • Makisio ya thamani ya uchumi utakaoingia Ohio: $200 million
  • Mkutano wa kwanza wa uteuzi wa chama cha Republican ulikuwa: Pittsburgh, Pa., 1856

Akielekea katika uteuzi huo Trump aliburuza watu na makundi mbali mbali na pia kuudhi makundi kadha kuanzia waislamu, wanawake, watu wenye ulemavu hadi wamarekani weusi.

Jukwaa kuu la mkutano wa Republican, Cleveland, Ohio
Jukwaa kuu la mkutano wa Republican, Cleveland, Ohio

Inaelekea makundi yote hayo atakuwa Cleveland pia wiki hii kufanya maandamano ya kumpinga Trump huku wanaomwunga mkono tajiri huyo nao wakijitokeza kwa wingi kuonyesha nguvu zake. Kuwepo kwa makundi yote hayo kunawatia wasiwasi maafisa usalama kwamba inawezekana matukio ya ghasia yakatanda katika mkutano huo wa siku nne.

Maafisa wa serikali kuu, jimbo na miji wameongeza ulinzi kuzungukia mkutano huo na wiki moja baadaye katika mkutano mkuu wa chama cha Democratic mjini Philadelphia hasa kufuatia matukio ya mashambulizi dhidi ya polisi Julai 7 huko Dallas, Texas, na Jumapili Julai 17, katika mji wa Baton Rouge, Louisiana.

Kiasi cha watu elfu 50 wanatazamiwa kuwa Cleveland baina ya Julai 18-21, na wiki moja baadaye maelfu wengine watakuwa Philadephia kwa ajili ya uteuzi wa Hillary Clinton na chama cha Democratic.

XS
SM
MD
LG