Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 10:49

Rishi Sunak ameidhinishwa kuwa waziri mkuu Uingereza


Rishi Sunak wakati alipozindua kampeni yake kugombea uongozi wa chama cha Conservative, London, Julai 12, 2022.
Rishi Sunak wakati alipozindua kampeni yake kugombea uongozi wa chama cha Conservative, London, Julai 12, 2022.

Waziri wa amani wa fedha nchini Uingereza, Rishi Sunak, ameteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha Conservative, na sasa antarajiwa kuchukua uongozi wa nchi hiyo kama waziri mkuu.

Sunak, anakabiliwa na kibarua kizito cha kusuluhisha mgogoro ndani ya chama na wa kiuchumi ambao umeikumba Uingereza.

Anakuwa waziri mkuu wa tatu kuingia madarakani ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, baada ya kujiuzulu kwa Boris Johnson na Liz Truss ambaye alijiuzulu baada ya siku 45 ofisini.

Ushindi wa Sunak, umetangazwa baada ya kujiondoa kwa mshindani pekee Penny Mordaunt aliyeshindwa kupata uungwaji mkono wa chama.

Sunak alishindwa na Liz Truss katika uchaguzi wa awali, lakini sasa, chama chake kimeonekana kuwa na imani naye kuliko wagombea wengine, kukabiliana hali ya kudorora kwa uchumi, mfumuko wa bei, na kuongezeka kwa bei ya nshati.

Ameahidi kwamba ataiongoza Uingereza kwa kuzingatia uadilifu, weledi na uwajibikaji. Amewaambia wanasiasa wa upinzani kwamba hakutakuwa na uchaguzi wa mapema kama chama cha Labour kilivyokuwa kimesema.

Sunak, ambaye ni mhindi wa kwanza kuwa waziri mkuu wa Uingereza, na mwenye umri wa chini kabisa wa miaka 42, anasubiri mfalme wa Uingereza Charles wa 3 kumuomba kuunda serikali.

XS
SM
MD
LG