Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:03

Mataifa ya Afrika kutokomeza malaria ifikapo 2020


Mtoto ambaye anaugua malaria na utapiamlo akiwa amelala kitandani katika hospitali mjini Bor, Sudan Kusini.
Mtoto ambaye anaugua malaria na utapiamlo akiwa amelala kitandani katika hospitali mjini Bor, Sudan Kusini.

Katika kipindi cha miaka minne ijayo, mataifa sita ya Afrika kwenye eneo ambalo malaria imeshamiri huenda lisiwe na ugonjwa huo, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema katika ripoti yake iliyochapishwa leo Jumatatu kuadhimisha siku ya malaria duniani.

“Mkakati wa kiufundi kwa ajili ya malaria duniani kwa 2016-2030” uliidhinishwa mwaka jana na WHO, ikitumaini kuona kumalizika kwa maambukizo ya malaria katika eneo katika takribani nchi 10 ifikapo mwaka 2020, lakini hivi sasa WHO inakadiria kwamba nchi 21 zitaweza kufanikisha lengo hilo, ikiwemo sita katika bara la Afrika.

Tangu mwaka 2000, vifo vya malaria vimeshuka kwa asilimia 60 duniani. Katika kanda ya Afrika, WHO imeeleza katika taarifa iliyoambatana na ripoti hiyo kuwa vifo vya malaria vilishuka kwa asilimia 66 miongoni mwa makundi ya rika zote na kwa asilimia 71 miongoni mwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Mataifa sita katika bara la Afrika ambayo huenda yakatokomeza malaria ifikapo mwaka 2020 ni Comoro, Afrika Kusini, Swaziland, Botswana, Algeria na Cape Verde

​
XS
SM
MD
LG