Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:24

Waziri mkuu wa zamani wa Australia atetea vita ya Iraq


Waziri Mkuu wa zamani, Tony Blair, azungumzia ripoti ya Iraq ya Uingereza, July 6, 2016
Waziri Mkuu wa zamani, Tony Blair, azungumzia ripoti ya Iraq ya Uingereza, July 6, 2016

Waziri Mkuu wa zamani wa Australia amejiunga na viongozi wengine wa nchi za magharibi leo kutetea uamuzi wao wa kwenda vitani na Iraq miaka 13 iliyopita.

John Howard, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Australia iliyopeleka wanajeshi elfu mbili nchini Iraq, alisema anatetea uamuzi huo na kamwe hatarudi nyuma.

Ripoti iliyotolewa Uingereza wiki hii ilisema kuwa uvamizi wa Iraq mwaka 2003 haukuwa wa lazima na Saddam Hussein hakuwa tishio kwa Uingereza au nchi nyingine za magharibi.

Uchunguzi uliongozwa na Afisa wa zamani wa Uingereza, John Chilcot, uliwalaumu vikali wanasiasa, maafisa wa kijasusi, wanadiplomasia na majenerali wa jeshi kwa kuipeleka Uingereza katika uvamizi huo ulioongozwa na Marekani – na pia vitendo vya majeshi ya Uingereza hasa kusini mwa Iraq.

Jumatano Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza alikubali lawama lakini akasisitza kuwa dunia iko katika hali nzuri zaidi baada ya kuondolewa kwa Saddam Hussein.

XS
SM
MD
LG