Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:25

Ripoti yaeleza haikuwa sahihi Uingereza kushiriki vita ya Iraq


Kiongozi wa jopo lililobuniwa kuchunguza jukumu la Uingereza kwenye vita vya Iraq mapema leo ametoa ripoti kuwa hatua ya kuingia kwenye vita hivyo haikuwa sawa na kwamba athari zake zinashuhudiwa hadi leo Jumatano.

John Chilcot aliewahi kuhudumu kwenye Serikali ameyasema hayo wakati akitoa ripoti baada kukusanya maoni kutoka kwa umma kwa miaka kadhaa na pia baada ya upekuzi wa nyaraka 150,000.

Jopo hilo lilikuwa linajaribu kutathmini iwapo vita hivyo vilivyoongozwa na Marekani vilikuwa na maana yoyote na kama athari zake zilikuwa zimezingatiwa kabla.

Chilkot ameongeza kusema hatua ya kushambulia Iraq ilikuwa muhimu kwa wakati mmoja, lakini Machi 2003, hakukuwa na tishio lolote kutoka kwa Saddam Hussein. Kufikia sasa, hakuna silaha zozote za mauwaji ya halaiki zilizopatikana Iraq.

XS
SM
MD
LG