Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:04

Thailand yaridhishwa na ripoti ya Marekani


Waziri wa Mambo za Nje wa Thailand, Don Pramudwinai
Waziri wa Mambo za Nje wa Thailand, Don Pramudwinai

Serikali ya Kijeshi ya Thailand imefurahishwa na matokeo ya ripoti ya kila mwaka ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani inayoorodhesha biashara harau ya watu TIP kwamba nchi hiyo imepanda juu kutokana na kuimarisha juhudi zake za kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu.

​Hata hivyo, Maafisa wa Myanmar wanalalamikia kwamba nchi yao imeshushwa chini katika orodha hiyo. Kulingana na ripoti hiyo, Thailand imepanda kutoka kundi la tatu hadi kundi la 2 ikimaanisha kwamba nchi baado haijafikiwa viwango vya wastani vya kutokomeza biashara haramu ya binadamu lakini imefanya maendeleo muhimu mwaka uliyopita.

Waziri Mkuu Prayuth Chan Ocha, Mkuu wa Baraza Tawala la Kijeshi, aliwambia waandishi wa habari kwamba sera ya kutovumilia biashara hiyo itaendelea naye ndiye ataiongoza kazi hiyo.

Ripoti hiyo ya TIP mwaka 2016 inaitaja Myanmar kua taifa ambalo wanaume wanawake na watoto wa nchi hiyo wanalazimika kufanya kazi kwa lazima na wanawake na watoto kukabiliwa na biashara ya ngono.

XS
SM
MD
LG