Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:10

Ripoti ya maendeleo ya binadamu Afrika


Abiria wasubiri kupanda taxi katika kitongoji cha Soweto kusini magharibi ya Johannesburg
Abiria wasubiri kupanda taxi katika kitongoji cha Soweto kusini magharibi ya Johannesburg

Nchi za Afrika zilizo chini ya jangwa la Sahara ndizo zimeathirika zaidi na baa la njaa

Licha ya hatua nzuri za kimaendeleo zilizofikiwa barani Afrika katika sekta ya uchumi wa-afrika wengi bado wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Katika uzinduzi wa ripoti ya maendeleo ya binadamu barani Afrika iliyotolewa Jumanne mjini Nairobi, Rais wa Kenya Mwai Kibaki, alieleza hali ya kusikitisha juu ya uhaba wa chakula katika bara hilo.

Rais huyo alisema nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara ndizo zimeathirika zaidi huku ikikisiwa watu milioni 239 wanaowakilisha asilimia 30 ya idadi ya watu hukabiliwa na baa la njaa mara kwa mara pamoja na utapiamlo.

Alisema zaidi ya watoto asilimia 38 wa Afrika wanaugua maradhi ya utapiamlo. Lakini chumi za bara hilo zinaonyesha kukuwa kwa asilimia 5 ukuaji mzuri miongoni mwa chumi zinazokuwa vyema duniani tangu mwaka wa 2010 na hali hiyo inabashiriwa kuendelea.

Ripoti hii iliyotolewa Jumanne mjini Nairobi Kenya ni ya kwanza barani Afrika kutolewa juu ya maendeleo ya kibinadamu kwa mwaka wa 2012. Kauli mbiu yake ilikuwa ‘kuelekea uthabiti wa chakula katika siku za baadaye’.

Ripoti hiyo ilielezea kutokuwa na uthabiti wa chakula kuwa na maana ya kukosa chakula cha kutosha mara kwa mara chenye lishe bora kwa afya na maisha bora.

XS
SM
MD
LG