Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:58

Ripoti ya Global Nutrition yaeleza lishe duni inaumiza watu na sayari


Wagonjwa walio na uzito kupita kiasi wakipata chakula katika kituo cha Aimin Fat Reduction huko Tianjin, China, Julai 24, 2008.
Wagonjwa walio na uzito kupita kiasi wakipata chakula katika kituo cha Aimin Fat Reduction huko Tianjin, China, Julai 24, 2008.

Takriban nusu ya idadi ya watu duniani wanakabiliwa na lishe duni inayohusishwa na chakula kingi au siyo chakula cha kutosha, tathmini ya kimataifa ilieleza Jumanne yenye athari kubwa kwa afya na sayari.

Matokeo ya uchunguzi wa dunia yamebaini kwamba takriban nusu ya idadi ya watu duniani wanakabiliwa na lishe duni inayohusishwa na chakula kingi kisicho bora au chakula kisitchotosha, na kusababisha athari kubwa kwa afya na dunia yetu.

Ripoti ya Global Nutrition Report (GNR), utafiti wa kila mwaka na uchambuzi wa data ya hivi karibuni kuhusu lishe na masuala yanayohusiana na afya, iligundua kuwa asilimia 48 ya watu kwa sasa wanakula kidogo sana au kupita kiasi na kusababisha unene kupita kiasi, au uzito mdogo sana.

Kwa viwango vya sasa, ripoti hiyo imegundua, dunia itashindwa kufikia malengo manane kati ya tisa ya lishe yaliyowekwa na Shirika la Afya Ulimwenguni kwa mwaka 2025.

Hii ni pamoja na kupunguza kuugua kwa watoto (wakati watoto ni wembamba sana kwa urefu wao) na kudumaa kwa watoto (wakati ni wafupi sana kwa umri wao), na pia unene kwa watu wazima.

Ripoti hiyo inakadiria kuwa karibu watoto milioni 150 walio chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa, zaidi ya milioni 45 ni ni wembamba sana kwa urefu wao na karibu milioni 40 wana uzito uliopitiliza.

XS
SM
MD
LG