Dr. Anthony Fauci amewaambia waandishi wa habari wa sauti ya Amerika VOA jana kuwa vijidudu vinavyokuwepo wakati wa kipindi cha awali cha maambukizo ya HIV ni tofauti na vile virusi vilivyosalia baada ya kipindi kirefu. Fauci, ambaye ni mkurugenzi wa magonjwa ya kuambukiza katika taasisi ya taifa ya afya nchini Marekani amesisitiza juu ya kuwepo kwa matibabu ya mapema dhidi ya ugonjwa huo katika kipindi ambacho hujakomaa. Fauci anatarajiwa kutoa mada juu ya ugonjwa huo wa Ukimwi katika mkutano wa kimataifa wa 18 wa Ukimwi nchini Austria wiki ijayo.
Afisa wa juu wa idara ya afya ya Marekani amesema dakika chache za awali baada ya maambukizo ya virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi zinaweza kuwa ni hatua muhimu ya kutoa nafasi ya kuzuia virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi kujikita katika mwili wa binadamu.