Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:45

Sakata la barua pepe za Clinton linaendelea


Ripoti iliovuja kutoka Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema kuwa waziri wa zamani wa wizara hiyo Hillary Clinton alikiuka maadili ya kikazi kwa kutumia anwani ya kibinafsi kusoma na kuandika barua pepe za kikazi wakati akiwa waziri wa mambo ya nje.

Ripoti hiyo ilikusudiwa kutolewa leo lakini ikavuja Jumatano. Afisa wa ngazi ya juu kutoka wizara hiyo anasema hakuna ushahidi kuwa Clinton aliomba idhini ya kutumia anwani binafsi na hata kama angeomba, hangeruhusiwa kufanya hivyo.

Maafisa wa Serikali wanatakiwa kutumia anwani za serikali kwa sababu za kiusalama na pia kuhifadhi rekodi za Serikali. Ripoti hiyo imeangazia matumizi ya barua pepe ya Waziri alieko sasa, John Kerry, na wengine waliomtangulia Clinton kama Condoleezza Rice, Colin Powell na Madeline Albright.

Ripoti hiyo imefichua kasoro za muda murefu lakini imeangazia swala la Clinton kwa kina zaidi.

XS
SM
MD
LG