Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 21:30

Riporti ya kuuliwa kwa raia 85 na ndege isiyo na rubani ya Nigeria itatolewa karibuni


Mwanafunzi aliyekuwa ametekwa nyara akiwa na mtoto wake katika kambi ya jeshi ya Maimalari huko Maiduguri Nigeria Juni 21, 2022. Picha na Audu MARTE / AFP
Mwanafunzi aliyekuwa ametekwa nyara akiwa na mtoto wake katika kambi ya jeshi ya Maimalari huko Maiduguri Nigeria Juni 21, 2022. Picha na Audu MARTE / AFP

Mkuu wa ulinzi wa Nigeria Jenerali Christopher Musa amesema siku ya Jumanne kuwa ripoti inayohusu ndege ya jeshi isiyo na rubani iliyoua raia 85 huko kaskazini mwa jimbo la Kaduma mwezi Novemba itatolewa mwisho wa mwezi Februari.

Rais Bola Tinubu ailitoa amri ya uchunguzi wa kina ufanyike kufuatia shambulio hilo, ambalo liliwalenga wanamgambo na majambazi.

Jeshi la nchi kavu na lile la anga yalitakiwa kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka katika majimbo ya kaskazini-magharibi na kati, yanayotishiwa na magenge ya wahaliufu wenye silaha ambayo huwashambulia kwa risasi wakazi wa vijiji na kuwateka nyara. Jeshi pia linapambana na wanamgambo wa kiislamu huko kaskazini maskariki ya nchi.

“Tuko hapa kuwalinda raia wasio na hatia, siyo kuwashambulia. Kulikuwa na makosa, na kunayafanyia kazi matatizo hayo” Jenerali Musa aliwaambia waandishi wa habari huko Abuja.

“Ripoti iko tayari na itatolewa labda kabla ya mwisho wa mwezi huu. Tuliahirisha kidogo kwa kuwa imekuwa vigumu kupata majina wa waliojeruhiwa. ” aliongezea kusema mkuu wa ulinzi.

Jenarali Musa amesema taifa hilo la Afrika Magharibi linataka kutengeneza silaha wakati nchi nyingi zinasita kuiuzia silaha Nigeria kutokana na wasi wasi kuhusiana na haki za binaadamu. Hakuzitaja nchi hizo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters .

Forum

XS
SM
MD
LG